EVA STESHENI
Monday, 31 March 2014
MAUAJI SUDANI KUSINI
Waasi Sudani Kusini leo wamefanya shambulio la Duk na kuua raia 36 na kujeruhi 31, Serikali yathibitisha.
UKAWA WAFANYA UZINDUZI
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) jioni hii wanazindua kampeni ya kudai Katiba ya wananchi kwenye Uwanja wa Milongo, jijini Mwanza
Tuesday, 4 February 2014
KATIBA
Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria Tundu Lissu, kupitia ITV amesema ameshitushwa na ukimya wa vyombo vya Habari wa kutoendesha mijadala ya Katiba Mpya.
MCHUNGAJI CHRISTOPHER MTIKILA ANUSURIKA
Mchungaji Christopher Mtikila anusurika kuuwawa baada ya kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa na mzozo wa ardhi. Ashonwa nyuzi 3 kichwani.http://goo,gl/uBLvV4
MALI YA HAYATI MANDELA YATANGAZWA
Mali za Hayati Nelson Madiba Mandela zatangazwa, aliachia familia yake mali zake zenye thamani ya Dola milioni 4.1 sawa na Tshs 6 Bilioni. Soma zaidi.>>>http://goo.gl/XjaEVZ
UJANGILI NCHINI
UNDP itachangia fedha kufanikisha Operesheni Tokomeza Awamu ya Pili. Marekani, Ufaransa, China nazo kusaidia, Waziri Nyalandu athibitisha leo.
WHO yaonya
Shirika la Afya Duniani WHO limeonya kuhusu kuibuka kwa wimbi baya la maambukizi ya ugonjwa hatari wa Saratani kote Duniani. Soma zaidi.>>>http://goo.gl/jcNcH3
Subscribe to:
Posts (Atom)