Ni baadhi ya nyimbo ambazo nimeimba. Tafadhali sikiliza upate kujifunza,
ni mawazo yangu ambayo nimeyaweka kupitia muziki. Nishauri pia ili
niweze kuboresha huduma hii. Album yangu ya kwanza ya nyimbo za Injili
inaitwa "KWANINI TUSIPENDANE" ina nyimbo kumi. Kwa sasa naandaa Album
nyingine ya nyimbo nzuri na zenye kiwango cha ubora zaidi ambayo hivi
karibuni nitawataarifu majina ya nyimbo hizo kupitia blog hii na vyombo
vingine vya habari. Namwomba Mungu anisaidie nifikie malengo yangu
kupitia uimbaji. Pili, wimbo nilioimba kwa lugha ya kiingereza uinaitwa
"UNAMID WOMEN NETWORK SONG" wimbo huu niliimba nilipokuwa Sudani
nikishiriki Ulinzi wa Amani. Aidha, pata kusikia wimbo unaokwenda kwa
jina la MTOTO WA KIKE wimbo huu ni maalum kwa ajili ya kutetea haki za
watoto wa kike, jamii ielewe kuwa mtoto wa kike ukimwendeleza atakufaa
kama ilivyo kwa mtoto wa kiume akiendelezwa. JINGLE ni maalum kwa ajili
ya kuhamasisha jamii iepuke ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na
watoto. Ujumbe huo umetolewa na Jeshi la Polisi Tanzania kupitia Dawati
la Jinsia na Watoto. Wapendwa, napenda kuwajulisha kuwa naandaa Album ya
nyimbo za kumtetea mtoto.
Kwanini tusipenda - Yalaeva
No comments:
Post a Comment