Tuesday, 4 February 2014
KATIBA
Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria Tundu Lissu, kupitia ITV amesema ameshitushwa na ukimya wa vyombo vya Habari wa kutoendesha mijadala ya Katiba Mpya.
MCHUNGAJI CHRISTOPHER MTIKILA ANUSURIKA
Mchungaji Christopher Mtikila anusurika kuuwawa baada ya kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa na mzozo wa ardhi. Ashonwa nyuzi 3 kichwani.http://goo,gl/uBLvV4
MALI YA HAYATI MANDELA YATANGAZWA
Mali za Hayati Nelson Madiba Mandela zatangazwa, aliachia familia yake mali zake zenye thamani ya Dola milioni 4.1 sawa na Tshs 6 Bilioni. Soma zaidi.>>>http://goo.gl/XjaEVZ
UJANGILI NCHINI
UNDP itachangia fedha kufanikisha Operesheni Tokomeza Awamu ya Pili. Marekani, Ufaransa, China nazo kusaidia, Waziri Nyalandu athibitisha leo.
WHO yaonya
Shirika la Afya Duniani WHO limeonya kuhusu kuibuka kwa wimbi baya la maambukizi ya ugonjwa hatari wa Saratani kote Duniani. Soma zaidi.>>>http://goo.gl/jcNcH3
KOMBO AAPISHWA ZANZIBAR
Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu A. Kificho asubuhi hii amwapisha Mahmoud T. Kombo kuwa mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki
IKULU YASEMA
Ikulu yasema Raisi hataidhinisha ombi la kuongeza kiinua mgongo cha wabunge wakistaafu kutoka milioni 43 hadi milioni 160 kama walivyoomba.
Soma zaidi.>>>http://goo.gl/DE2xsU
Soma zaidi.>>>http://goo.gl/DE2xsU
BIASHARA ZA KIMATAIFA
Serikali mwezi huu kujadili report TZ kushuka viwango vya Biashara, Waziri wa Viwanda, Biashara Dr. Kigoda asema punde kupitia Radio One
WHO YAONYA
Kesi mpya ya Saratani Duniani kufikia 25 Milioni kwa mwaka ifikapo 2032, zapaa toka 12 M mwaka 2008 - 2014 M mwaka 2012. WHO yataka mabadiliko staili za maisha.
BALAA NJAA
UN yaomba Dola za Kimarekani 2 Bilioni kuhudumia watu 20 Milioni wa ukanda wa Sahel unaojumuisha Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati. 2.5 M wanahitaji msaada wa dharura
RUSHWA EU
Ripoti yaonesha uchumi Umoja wa Ulaya umeathiriwa vibaya na rushwa , Dola za Kimarekani 162 Bilioni zapotea kila mwaka. Ugiriki ni kinara, Denmark ahueni.
Subscribe to:
Posts (Atom)