Slider

Monday, 31 March 2014

MAUAJI SUDANI KUSINI

Waasi Sudani Kusini leo wamefanya shambulio la Duk na kuua raia 36 na kujeruhi 31, Serikali yathibitisha.

UKAWA WAFANYA UZINDUZI

Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) jioni hii wanazindua  kampeni ya kudai Katiba ya wananchi kwenye Uwanja wa Milongo, jijini Mwanza

Tuesday, 4 February 2014

KATIBA

Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria Tundu Lissu, kupitia ITV amesema ameshitushwa na ukimya wa vyombo vya Habari wa kutoendesha mijadala ya Katiba Mpya.

MCHUNGAJI CHRISTOPHER MTIKILA ANUSURIKA

Mchungaji Christopher Mtikila anusurika kuuwawa baada ya kushambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa na mzozo wa ardhi. Ashonwa nyuzi 3 kichwani.http://goo,gl/uBLvV4

MALI YA HAYATI MANDELA YATANGAZWA

Mali za Hayati Nelson Madiba Mandela zatangazwa, aliachia familia yake mali zake zenye thamani ya Dola milioni 4.1 sawa na Tshs 6 Bilioni. Soma zaidi.>>>http://goo.gl/XjaEVZ

UJANGILI NCHINI

UNDP itachangia fedha kufanikisha Operesheni Tokomeza Awamu ya Pili. Marekani, Ufaransa, China nazo kusaidia, Waziri Nyalandu athibitisha leo.

WHO yaonya

Shirika la Afya Duniani WHO limeonya kuhusu kuibuka kwa wimbi baya la maambukizi ya ugonjwa hatari wa Saratani kote Duniani. Soma zaidi.>>>http://goo.gl/jcNcH3

KOMBO AAPISHWA ZANZIBAR

Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu A. Kificho asubuhi hii amwapisha  Mahmoud T. Kombo kuwa mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki

IKULU YASEMA

Ikulu yasema Raisi hataidhinisha ombi la kuongeza kiinua mgongo cha wabunge wakistaafu kutoka milioni 43 hadi milioni 160 kama walivyoomba.
Soma zaidi.>>>http://goo.gl/DE2xsU

BIASHARA ZA KIMATAIFA

Serikali mwezi huu kujadili report TZ kushuka viwango vya Biashara, Waziri wa Viwanda, Biashara Dr. Kigoda asema punde kupitia Radio One

WHO YAONYA

Kesi mpya ya Saratani Duniani kufikia  25 Milioni kwa mwaka ifikapo 2032, zapaa toka 12 M mwaka 2008 - 2014 M mwaka 2012. WHO yataka mabadiliko staili za maisha.

BALAA NJAA

UN  yaomba Dola za Kimarekani 2 Bilioni kuhudumia watu 20 Milioni wa ukanda  wa Sahel unaojumuisha Sudan, Jamhuri ya Afrika ya Kati. 2.5 M wanahitaji msaada wa dharura

RUSHWA EU

Ripoti yaonesha uchumi Umoja wa Ulaya umeathiriwa vibaya na rushwa , Dola za Kimarekani 162 Bilioni zapotea kila mwaka. Ugiriki ni kinara, Denmark ahueni.

Thursday, 30 January 2014

NAMNA YA KUEPUKA UGONJWA WA KIHARUSI

Namna au jinsi ya kuepuka ugonjwa wa Kiharusi;
1. Kuwa na uzito usiozidi kiasi
2. Epuka matumizi ya Pombe.
3. Usivute sigara
4. Kapime kiasi cha sehemu (cholesterol) mwilini mwako
5. Kapime sukari mwilini mwako
6. Kuwa mwangalifu upande wa chakula.
7. Pungunza matumizi ya chumvi
 8. Fanya mazoezi ya mwili
9. Matumizi sahihi ya dawa ni muhimu
Soma zaidi,>>>http://goo.gl/nOCFsG

HUKUMU YA KIFO

Serikali ya Marekani yataka hukumu ya kifo dhidi ya DZHOKHAR TSARNAEV mtuhumiwa wa shambulio la Bomu Boston mwaka jana, liliua 3 na kujeruhi 260.

MABOMU MSIBANI

Mabomu yarindima usiku Musoma mjini kwa aliyekuwa Shekhe Mkuu Mara, marehemu Othman Magee kutuliza wafuasi wa Dr. Slaa na V. Mathayo wa CCM.

UTAFITI

Unywaji mwingi wa Pombe unaweza kuleta hisia zisizo za kawaida mwilini ambazo zinaweza kuleta Saratani ya ngozi. Soma zaidi.>>>http://goo.gl/Mki1V0

SADC YAIONDOLEA VIKWAZO MADAGASCAR

Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) imeiondolea vikwazo Madagascar baada ya kufanyika kwa uchunguzi wa kidemocrasia hivi karibuni.
Soma zaidi.>>>http://googl/7ttWi7

MIRADI YA NISHATI

Shirika la umeme Tanzana TANESCO lasema uwekezaji utafikia dola za Kimarekani 15 Bilioni miaka michache ijayo kutoka Bilioni 4. Wengi kunufaika unafuu wa bei ya umeme

HATII BANDIA

Watu 9 akiwemo Afisa wa Jeshi la Polisi, mfanyakazi shirika la ndege la Kenya wakamatwa wakihushwa na mtandao wa kupitisha watu wenye hati feki za kusafiria.

BANDARI BUBU

Serikali imeanza mchakato wa kuzipandisha hadhi Bandari bubu za Jasini, Kigombe na Mkwaja mkoani Tanga ili kudhibiti magendo na wahamiaji haramu.

LENOVO YANUNUA KAMPUNI YA SIMU YA MOTOROLA

Kampuni ya vifaa vya kiteknolojia ya LENOVO imenunua kampuni ya simu ya MOTOROLA iliyokuwa ikimilikiwa na GOOGLE kwa dola za Kimarekani biliono 2.91. na kuifanya kuwa kampuni kubwa kabisa ya nne ya Kichina kufanya
manunuzi ya aina hiyo.

Manunuzi haya yataiwezesha Lenovo kupanua soko lake kutoka China na kupenya kwenye masoko ya Marekani ambapo simu za Kichina zimekosa soko na pia kuchimbia mizizi soko la Motorola lililoshamiri Amerika ya Kusini.

Kwa mujibu wa takwimu za Lenovo na IDC, sehemu ya Lenovo kwenye soko itakuwa asilimia 6, wakati Samsung tayari ina asilimia karibu 29 huku Apple ikishikilia asilimia karibu kumi na nane.

Google imelazimika kuuza kilicho chake kutokana na msukosuko wa kiusalama kampuni hiyo inaoupata nchini China kwenye mawasiliano ya mitandao yake.Soma zaidi.>>> http:/goo.gl/tebwo0

MCHEZAJI YAYA TOURE, MWANAMUZIKI D'BANJ NA RAISI KIKWETE WAUNGANA

Mchezaji Yaya Toure, mwanamuziki D'banj na Raisi Kikwete waungana kwenye kampeni ya kuhimiza kilimo ili kuondoa umasikini.
Soma zaidi.>>>http://goo.gl/pmpTny

MWANAMUZIKI MASHUHURI JUSTIN BIEBER AMEFUNGULIWA MASHITAKA

Mwanamuziki JUSTIN BIEBER maarufu ulimwenguni amefunguliwa mashitaka ya kumpiga dereva wa gari la kifahari aliloliikodisha mwezi December mwaka jana.
Soma zaidi.>>>http://goo.gl/31mWUI

DR. JUMA NGASONGWA ANUSURIKA

Dr. Juma Ngasngwa anusurika katika ajali ya gari Picha ya Ndege, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Gari lake laharibika vibaya sana.
Soma zaidi.>>>http://goo.gl/j64lMe

Tuesday, 28 January 2014

MORSI MAHAKAMANI

Raisi aliyepinduliwa nchini Misri mwaka 2013 Mohamedi Morsi afikishwa mahakamani jijini Cairo. Serikali yasema anakabiliwa na makosa manne tofauti.

WAKULIMA 4000 WANUFAIKA MKOANI MOROGORO

Zaidi ya wakulima 4000 mkoani Morogoro wanufaika fa fedha kiasi cha Milioni 800 zilizotolewa na mfuko wa AGRA. Soma zaidi.>>>http://goo.gl/MafCb1

CHADEMA YAPONGEZA KAZI ZA MBUNGE WA CCM

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepongeza kazi za mbunge wa CCM wa jimbo la Korogwe vijijini MHE Steven Ngonyani almaarufu kama Profesa Maji Marefu. Ni katika kutatua matatizo ya wananchi jimboni kwake. Soma zaidi.>>>http://goo.gl/OOzTqX

BREAKING NEWS

Mwigizaji maarufu wa vichekesho katika kundi la Futuhi mzee Dude amefariki Dunia.
Soma zaidi,>>>http://goo.gl/Q3afFG

WANAFUNZI 355 WANUSURIKA

Wanafunzi 355 wa shule ya Sekondari Wenda iliyopo Mbalizi mkoani Mbeya wamenusurika kifo baada ya Mabweni 4 wanayoyatumia kuteketea kwa moto. Polisi Mbeya yathibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo asubuhi. Wanafunzi hawakuwepo Bwenini. Chanzo hakijajulikana.

MAGAIDI YABANWA

UN yapitisha azimio kuyataka mataifa kutoyalipa makundi ya kigaidi kwa kushikilia Mateka, UK yasema yameingiza 105M miaka 3 na nusu iliyopita.

KITUKO

Dr. wa Chuo Kikuu Dar es Salaam  ashushwa kwenye ndege ya Precision Air alipohoji ni kwa nini asipewe maelezo katika lugha ya Kiswahili.
Soma zaidi.>>>http://goo.gl/glSLm9

UCHAGUZI MISRI

Huku jeshi likimbariki bosi wake, ABDEL FATAH AL - SISI kuwania uraisi katika uchaguzi ujao. Raisi A. MANSOUR ampandisha cheo jana kuwa Field Marshal

UGAIDI NIGERIA

Polisi nchini Nigeria wathibitisha watu 20 kufa kwenye mlipuko wa bomu jana jioni katika katika kijiji cha Borno; Boko Haram wahusishwa na tukio hilo

Monday, 27 January 2014

SAMWEL SITTA AWASIHI VIJANA

Mhe. Samwel Sitta (MB) na Waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki amewasihi vijana kutokuwa waoga wa rasilimali za nchi. Asema kuna viongozi wanataka kuhodhi madaraka ili wajinufaishe wao.
Soma zaidi.>>>http://goo.gl/b7Wl5e

BOTI YAZAMA INDIA .

Watalii 21 wakihindi wafa maji jumapili baada ya Boti walikua wameipanda kuzama katika pwani ya visiwa vya Andaman, Nicobar. Upelelezi kubaini chanzo cha ajali waanza.

MGOMO NZEGA

Mabasi ya abiria yameruhusiwa kuendelea na safari zake jana jioni baada ya kugoma tangu juzi usiku mjini Nzega Tabora, RPC Peter Ouma amethibitisha.

WANARIADHA KENYA WANATISHIA

Wanariadha nchini Kenya wanatishia kutoiwakilisha nchi yao kwenye michezo ya Olympiki mwaka 2016 ikiwa serikali itaamua waanze kulipa kodi.
Soma zaidi.>>>http://goo.gl/0rnuHA

KWA MARA YA KWANZA MAHASIMU WA SYRIA WANATARAJIWA KUKUTANA

Kwa mara ya kwanza mahasimu wa Syria wanatarajiwa kukutana leo hii katika mazungumzo ya amani yanayoendelea mjini Geneva. Soma zaidi.>>>http://goo.gl/6lGSds

HAYA NDIO MATOKEO YA WIZI

Kijana mmoja apigwa risasi na kufa papo hapo wakati akijaribu kuiba kwenye kituo cha gesi.
Soma zaidi.>>>http://goo.gl/kYn0ro

BILIONEA WA CHINA AONGEZA DAU

Bilionea wa China aongeza dau kwa mwanaume atakayemwachisha binti yake usagaji. Aaahidi Bilioni 194 kama zawadi. Soma zaidi.>>>http://goo.gl/CMEDXL

TUMIA NJIA ZA ASILI KUONDOA MADOA USONI

Paka mchanganyiko wa Papai na Asali usoni kwa dakika 10 mpaka 15 baada ya kuusafisha kwa maji.
Soma.>>>http://goo.gl/4q1d2E

KITUKO

Baba aamua kumshitaki mwanawe kwa kuoa mwanamke masikini. Asema amemuharibia sifa yake.
Soma  zaidi >>>http://goo.gl/fwHLsy

Friday, 24 January 2014

AJALI TABORA

Dereva basi la Taqwa linalosafiri kati ya Dar es Salaam na Burundi amekufa, watu 10 wajeruhiwa baada ya kugongana uso kwa uso na lori eneo la Miguwa, Nzega jana

MAFURIKO DUMILA

Ukarabati wa daraja umekamilika , malori yameruhusiwa kupita hivi punde. Serikali yasema magari madogo na mabasi kuendelea kutumia njia mbadala.

MTANZANIA MWENYE ULEMAVU AZUNGUKA MAREKANI, ULAYA NA AFRIKA

Mtu mmoja mwenye uraia wa Tanzania amezunguka Marekani, Ulaya na Afrika kwakutumia baiskeli kuchangisha fedha kwa ajili ya Elimu. Sasa yupo Liberia.
Soma zaidi hapa>>>>http://goo.gl/2aglZz

RUSHWA YA NYAMA

Afisa mifugo, mkaguzi wa nyama Singida Edwin Mtae apanda kortini leo akituhumiwa kuomba rushwa ya nyama. Amedhaminiwa kesi kundelea February 6.

RAISI KIKWETE AKIWA NA NAIBU RAISI WA KENYA MHE. WILLIAM RUTO

Raisi Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa baadhi ya viongozi wa Kenya na Makamu wa Raisi wa Kenya Mhe. William Ruto walipowasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata jijini Nairobi leo ijumaa January 24, 2014. Viongozi hawa walikutana jijini Amsterdam, Uholanzi na kupanda Ndege moja kuelekea nyumbani. Raisi Kikwete ambaye alitua Nairobi kwa muda alikua akitokea Davos, Uswisi alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ambayo ameikatisha ili kujiunga na wananchi wa jimbo la Chalinze katika msiba wa mbunge wa jimbo hilo Marehemu Saidi Bwanamdogo. Ambaye amefariki dunia January 22, 2014 katika wodi ya taasisi ya mifupa na fahamu (MOI) alipokuwa akitubiwa. Mazishi yamepangwa kufanyika leo nyumbani kwa marehemu Miono, Bagamoyo.

WALIMU WAVAMIWA:

Majambazi yavamia familia 3 za walimu S/M Tembomine, Geita alasiri leo na kucharanga watu mapanga. Polisi yasema 4 wamejeruhiwa, na kuibiwa mali.

MSANII DIAMOND AWAPELEKA WATOTO WAWILI SHULE YA KIMATAIFA.

Ni walioshinda katika tamasha lake aliloendesha sikukuu ya Chrismass
Soma hapa zaidi.>>>http://goo.gl/GWhgCM

HALI YA MWIGIZAJI MKONGWE BLANDINA CHAGULA "JOHARI"

Hali ya mwigizaji mkongwe Johari si nzuri hata kidogo amelazwa hoi hospitalini,
Soma zaidi hapa >>http://goo.gl/kk1CFw

KENYATTA NA ICC:

Mahakama yakimataifa ya ICC, imeahirisha kesi ya Raisi Uhuru Kenyatta iliyotarajiwa kuanza February 5, 2014. Yasema pande zote zikutane siku hiyo.

KUTUMIA SIMU USIKU KUNAHARIBU USINGIZI NA UTENDAJI WA KAZI SIKU INAYOFUATA

Mwanga wake hupunguza  uzalishwaji wa kemikali ya usingizi .
http://goo.gl/WgbMRv

RAISI WA KLABU YA BARCELONA SANDRO ROSELL AMEJIUZULU

Kufuatia madai ya matumizi mabaya ya fedha wakati wa usajili wa Neymar.
Soma hapa >>> http://goo.gl/nWd2Aa

MLIPUKO MISRI

Waua watu 4 na kujeruhi wengine zaidi ya 30 karibu na makao makuu ya Polisi mjini Cairo asubuhi hii. Mamlaka zasema majengo yameharibiwa vibaya.

MAFURIKO DUMILA

Dkt. John Magufuli asema punde ukarabati wa daraja umekamilka, magari yataruhusiwa kupita masaa machache yajayo, malori 150 kunasuliwa kwanza.

MTOTO ALIYEPIGWA NA BABA YAKE NA KULAZWA AFARIKI DUNIA

Ni kutokana na majeraha aliyoyapata . Baba afikishwa mahakamani Jumatatu ijayo.
http://goo.gl/06gl0F

SHERIA YA UBAKAJI MORROCO KUREKEBISHWA

Ni ile inayomruhusu mwanaume aliyebaka kufutiwa kesi pindi akikubali kumuoa mwathirika
http://goo.gl/myHVfi

Thursday, 23 January 2014

MATUMAINI SUDANI KUSINI:

Serikali waasi wasaini makubaliano kusitisha vita punde huko Ethiopia, wapatanishi wasema zaidi ya laki 5 wameathiriwa na vita hiyo.