Slider

Friday, 24 January 2014

RAISI KIKWETE AKIWA NA NAIBU RAISI WA KENYA MHE. WILLIAM RUTO

Raisi Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa baadhi ya viongozi wa Kenya na Makamu wa Raisi wa Kenya Mhe. William Ruto walipowasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyata jijini Nairobi leo ijumaa January 24, 2014. Viongozi hawa walikutana jijini Amsterdam, Uholanzi na kupanda Ndege moja kuelekea nyumbani. Raisi Kikwete ambaye alitua Nairobi kwa muda alikua akitokea Davos, Uswisi alipokuwa kwenye ziara ya kikazi ambayo ameikatisha ili kujiunga na wananchi wa jimbo la Chalinze katika msiba wa mbunge wa jimbo hilo Marehemu Saidi Bwanamdogo. Ambaye amefariki dunia January 22, 2014 katika wodi ya taasisi ya mifupa na fahamu (MOI) alipokuwa akitubiwa. Mazishi yamepangwa kufanyika leo nyumbani kwa marehemu Miono, Bagamoyo.

No comments:

Post a Comment