Slider

Thursday, 30 January 2014

LENOVO YANUNUA KAMPUNI YA SIMU YA MOTOROLA

Kampuni ya vifaa vya kiteknolojia ya LENOVO imenunua kampuni ya simu ya MOTOROLA iliyokuwa ikimilikiwa na GOOGLE kwa dola za Kimarekani biliono 2.91. na kuifanya kuwa kampuni kubwa kabisa ya nne ya Kichina kufanya
manunuzi ya aina hiyo.

Manunuzi haya yataiwezesha Lenovo kupanua soko lake kutoka China na kupenya kwenye masoko ya Marekani ambapo simu za Kichina zimekosa soko na pia kuchimbia mizizi soko la Motorola lililoshamiri Amerika ya Kusini.

Kwa mujibu wa takwimu za Lenovo na IDC, sehemu ya Lenovo kwenye soko itakuwa asilimia 6, wakati Samsung tayari ina asilimia karibu 29 huku Apple ikishikilia asilimia karibu kumi na nane.

Google imelazimika kuuza kilicho chake kutokana na msukosuko wa kiusalama kampuni hiyo inaoupata nchini China kwenye mawasiliano ya mitandao yake.Soma zaidi.>>> http:/goo.gl/tebwo0

No comments:

Post a Comment